Kalori ni kipimo cha nishati, katika
lishe na lugha ya kawaida, Kalori ni matumizi ya nishati katika chakula na
vinywaji na matumizi ya nishati ya mwili katika shughuli za kawaida za mwili.
Kwa mfano, tunda la apple linaweza kuwa na kalori 80, lakini kutembea kilomita
moja kunaweza kutumia mpaka kalori 100
Aina za kalori:
·
Kalori ndogo (Alama :cal)- ca 1 ni
kiasi cha nishati kinachohitajika kunyanyua gramu moja ya maji kwa digrii moja
ya Celsius.
·
Kalori(Alama: kcal)- Kca 1 ni kiasi
cha nishati kinachohitajika kunyanyua kilogramu moja ya maji kwa digrii moja ya
Celsius
Watu wengi wanakosea wanapohusianisha Karoli katika chakula
na vinywaji, lakini kitu chochote kilicho na nichati kina kalori. Kwa mfano
tani moja ya makaa yam awe inaweza kuwa sawa na kalori 7,004,684,512
Kalori kubwa 1= kalori ndogo 1000
Kalori ambazo huandikwa katika lebo
za vyakula, huwa, kilokalori ambazao huwa na kiasi cha kalori ndogo 1000
Kwa nini kalori ni muhimu
kwa afya ya binadamu?
Mwili wa binadamu unahitaji nishati
ili uweze kuwepo katika hali ya kawaida, bila nishati katika mwili chembe hai
katika mwili huweza haribika na kufa, ikiwa hivyo moyo na mapafu vinaweza
simama kufanya kazi zake. Mwili unapata
nishati kutoka katika vyakula na vinywaji.
Kama tutatumia kiasi cha kalori
ambacho mwili unahitaji kila siku, hakika utafurahi kuwa na afya njema. Lakini
matumizi ya kalori katika mwili yapo chini sana au juu sana, bila shaka utapata
matatizo ya kiafya.
Kiasi cha Kalori ambacho kimo katika
chakula ni kiasi kinachotuonyesha nishati iliyomo katika chakula hicho. Hapa
chini kuna vipimo vya kalori katika aina kuu za
vyakula tunavyokula.- Gramu 1 ya wanga(carbs) ina kiasi cha kalori 4
- Gramu 1 ya protini ina kiasi cha kalori 4
- Gramu 1 ya mafuta(fats) ina kiasi cha karoli 9
Kiasi
gani cha kalori tunahitaji katika siku?
Si kila mtu anahitaji kiasi kile kele cha
kalori anachotumia siku moja katika siku
zote. Mahitaji yetu ya kalori katika mwili yanategemea mambo mbalimbali ikiwamo
afya ya mwili kiujumla, mahitaji ya mwili katika shughuli/kazi, jinsia, uzito,
kimo na umbile. Mfano mchezaji wa mpira wa umri wa miaka 25 mwenye urefu wa futi 6 anahitaji
kalori nyingi zaidi kuliko mwanamke wa miaka 50 mwenye urefu wa futi 5.
Mamlaka za afya mbalimbali duniani bado hazijakubali
kuhusu kiasi ambacho watu wao wanatakiwa watumie, mfano Marekani wao wanashauri
kwamaba mwanaume anatakiwa atumie kwa wastani kalori 2700 kwa siku na mwanamke
atumie wastani kalori 2200 kwa siku, wakati Uingeraza(nationa Health Service)
wanashauri ni 2500 na 2000 kwa mwanamke.
Wakati huo huo shirika la Kilimo na Chakula
Duniani(FAO) linasema mtu mzima anatakiwa asitumie chini ya kalori 1800 kwa
siku.


0 comments:
Chapisha Maoni