Mazoezi
ya mwili
Mazoezi ya mwili nishughuli yoyote ambayo inayouwezesha
mwili kuwa na utimamu wa mwili siha na afya njema ya mwili kiujumla katika utendaji wake. Hivyo ufanywaji wa
mazoezi ya mwili hufanyika kwa madhumuni ya kuboresha na kukarabati mifumo mbalimbali katika mwili
ili iweze kufanya kazi inavyotakiwa, kuboresha ujuzi wa kimichezo na
kuburudisha mwili na akili.
Faida za mazoezi ya Mwili
Mazoezi ya mwili ya mara kwa mara yanasaidia katika mambo
yafuatayo kama
·
Kuboresha mfumo wa kinga mwilini
·
Kupunguza magonjwa ya moyo na kuboresha
utendaji wa mfumo wa moyo na damu(CARDIOVASCULAR SYSTEM)
·
Kupunguza magonjwa ya mapafu na kuboresha mfumo
wa mapafu(PULMONARY SYSTEM)
·
Kuzuia magonjwa ya kisukari hasa ugonjwa
kisukari namba 2(type 2 diabet)
·
Kupunguza tatizo la unene kupita kiasi au
kiribatumbo (obesity)
·
Kuboresha afya ya akili na utendaji kazi wa
ubongo
·
Kupunguza msongo wa mawazo na mfadhaiko
·
Kumwezesha mtu kuwa na hali ya kujisikia kwa
kuwa na afya nzuri(self esteem)
Kwa ujumla mazoezi yanafaida nyingi sana
hasa katika kipindi hiki ambacho mfumo wa maisha ya watu umebadilika na
kupunguza utendaji kazi wa mwili wa kiasili kutokana na vyakula na shughuli za
kibinadamu hivyo kusababisha kiribatumbo/uzito na magonjwa mengine hatari.
Aina za mazoezi
Mazoezi ya mwili yamegawanyika katika
makundi matatu kutokana na matokeo mwili yanayofanyika katika mwili pindi
mazoezi hayo yanapofanyika
1.
Mazaoezi ya Aerobiki (Mazoezi yanayohusisha Oksijeni
nyingi)
Mazoezi
haya huusisha shughuli yoyote ambayo inatumia misuli mingi ya mwili na
kusabaisha matumizi makubwa ya oksijeni mwilini tofauti na hali ya kawaida .
Malengo
makubwa ya mazoezi haya ni kuongeza ustahimilivu wa utimamu wa mfumo wa
Moyo/mzunguko wa damu na mfumo wa Mapafu/hewa.
Mfano
wa mazoezi ya Aerobiki ni: kuendesha baiskeli, kuogelea, kutembea kwa kasi,
kukimbia, kuruka na kuvuta kamba, mazoezi ya viungo ya mwendelezo pamoja na
michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, tenisi n.k
2.
Mazoezi ya Anaerobiki (Mazoezi yasiyohusisha
matumizi ya Oksijeni nyingi)
Aina
hii ya mazoezi huitwa mazoezi ya nguvu au ukinzani katika mwili ambapo
huwezesha kuipa nguvu na uimara misuli na mifupa , kuratibisha uwiano wa
mwili na uratibu wa mfumo wa misuli.
Mfano
wa mazoezi haya ni: Mazoezi ya Msukumo(pushups), Mchuchumio(lunges),
kujivuta(pull-ups), kukimbia kasi(sprintings), kunyanyua na kuvuta vitu
vizito(weightlifting and rowing)
3.
Mazoezi ya Mnyumbuko(Flexibility)
Mazoezi
ya Mnyumbuko ni aina ya mazoezi ambayo huusisha unyumbuaji au uvutaji wa misuli
katika mwili ili kuwezesha ubadilikaji wa umbo la misuli katika mwili
unapofanya kitu chochote, mazoezi haya hupunguza majeraha katika misuli pindi
tendo lolote la kiutendaji la mwili katika mwendo linapofanyika.
Kwa
ujumla mazoezi ya mwili yanawezesha umakini(accuracy), wepesi wa
mwili(agility), nguvu(power) na Mwendokasi(speed) katika shughuli za kawaida za
binadamu na michezoni.

0 comments:
Chapisha Maoni